Taasisi Ya Kimataifa Inayoshughulikia Masuala Yaliyosalia Ya Mahakama Za Makosa Ya Jinai (Mechanism)Yaomboleza Kifo Cha Rais Magufuli

Mechanism
Arusha, Lahe
Mechanism deeply saddened by passing of President Magufuli

Taasisi Ya Kimataifa Inayoshughulikia Masuala Yaliyosalia Ya Mahakama Za Makosa Ya Jinai (Mechanism) Yaomboleza kwa masikitiko kifo cha Mh Dk John Pombe Magufuli Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania kilichotokea Jumatano ,17 Machi 2021.Inapenda kuungana na jumuiya ya kimataifa katika kutoa salaam za dhati za rambi rambi kwa familia ya Rais Magufuli,Makamu wa Rais Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan, Serikali na Watanzania

Rais Magufuli tutamuenzi kwa umahiri wake katika jukwaa la siasa Tanzania. Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama Mbunge mwaka 1995 na baada ya hapo amelitumikia taifa la Tanzania kwa nyadhifa mbali mbali ikiwemo kushika wadhifa wa Naibu Waziri wa Ujenzi toka mwaka 1995 hadi 2000 na baadaye Waziri wa Ujenzi kutoka mwaka 2000 hadi 2005. Kutoka mwaka 2006 hadi 2008 alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na Makazi ya Watu, Waziri wa Mifugo na Uvuvi mwaka 2008 hadi 2010 na tena kuteuliwa Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2015 Alipochaguliwa Rais wa Awamu ya Tano mwaka 2015, hatimaye kuanza kipindi chake cha pili mwezi Oktoba 2020.

Katika kipindi chake cha uongozi wa taifa la Tanzania, Rais Magufuli amewahi kushika wadhifa wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kuanzia mwaka 2019 hadi 2020

Katika muda wote wa Urais wa Magufuli (Mechanism) iliendelea kupokea mchango muhimu kutoka Tanzania ikiwemo ujenzi wa mahakama yake ya kudumu jijini Arusha. Mechanism inatarajia ushirikiano endelevu na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza majukumu yao.

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wataomboleza siku 14, bendera ya Umoja wa Mataifa itapeperushwa nusu mlingoti Mahakama yetu Arusha (yaani Mechanism) katika kipindi chote cha kuomboleza.